Sera ya Faragha

SERA YA FARAGHA

Kampuni yetu inaheshimu faragha ya taarifa zako binafsi. Taarifa zote unazotupatia (jina, namba ya simu, NIDA, mahali unapoishi, taarifa za wadhamini na picha yako) zitatumika tu kwa madhumuni ya kuchambua na kusimamia maombi ya mkopo wako.

Hatutashiriki taarifa zako na mtu wa tatu bila idhini yako, isipokuwa inapohitajika kisheria au kwa madhumuni ya kudai malipo ya mkopo.

Taarifa zako zitahifadhiwa kwa usalama na kutumika kwa muda unaohitajika tu kuhusiana na mkopo wako.

Kwa maswali yoyote kuhusu faragha ya taarifa zako, wasiliana nasi kupitia namba iliyoonyeshwa kwenye tovuti hii.

Vigezo na Masharti

VIGEZO NA MASHARTI YA MKOPO

1. Riba ya mkopo huanzia asilimia 30% kwa mwezi mmoja na huongezeka kadri muda wa mkopo unavyoongezeka.
2. Kila mwombaji anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye namba za simu zinazofanya kazi.
3. Taarifa za NIDA na picha ni lazima kwa uthibitisho wa utambulisho.
4. Malipo ya mkopo yanaweza kufanywa kidogo kidogo (malipo ya awamu) mpaka deni likamilike.
5. Kushindwa kulipa mkopo kwa muda uliopangwa kunaweza kupelekea gharama za nyongeza.
6. Kwa kukubali masharti haya, unathibitisha kuwa taarifa zote ulizotoa ni za kweli.